Men The Podcast

One of the major barriers to men addressing and tackling the challenges they face is the fact that discussion of mental health is largely taboo for Tanzanian men. They’re not expected to open up and talk about their struggles with life. Every two weeks (Fortnightly), on Wednesdays Michael Baruti and Nadia Ahmed present an episode that will discuss the challenges that men go through and offer detailed insight on mental health for men. If you’re interested in Mental Health and are interested in unpacking and unlearning mental health for men in Tanzania, this podcast is exactly what you need

https://www.menthepodcast.com

subscribe
share






episode 79: Jali afya yako ya akili


Mwezi wa kumi huwa ni mwezi maalumu kwa ajili ya kufanya kampeni inayokuza na kueneza uelewa kuhusu afya ya akili (Mental Health Awareness month). Na dhima kubwa ya mwaka huu inasema “Afya ya akili ni haki ya binadamu kwa wote


Kwa kujua umuhimu wa siku hii na namna gani swala zima la afya ya akili linavyohitaji mjadala mpana nchini Tanzania, Michael na Nadia wameketi chini na kuichambua safari nzima ya afya ya akili hapa nchini Tanzania.


Tunakubaliana na ukweli kwamba kuna hatua zimepigwa kwenye kuhakikisha misaada na ufahamu wa afya ya akili unaongezeka katika jamii, ila lazima tuwe wakweli kwamba bado pengo pia linaonekana. 


Mazungumzo ya leo  yanatulezea namna ya kugundua changamoto za afya ya akili, umuhimu wa kutafuta msaada, msaada unapopatikana lakini pia, kama hauwezi kumudu gharama za wataalamu, ni nini ambacho unaweza kiufanya mwenyewe ili uweze kujiokoa?


Mazungumzo yote ya leo yamefanyika yakiwa na lengo moja tu, kukufanya uanze kujali afya yako ya akili. Na ndiyo maana kipindi cha leo kinaitwa “Jali afya yako ya akili”


fyyd: Podcast Search Engine
share








 October 19, 2023  1h8m