Men The Podcast

One of the major barriers to men addressing and tackling the challenges they face is the fact that discussion of mental health is largely taboo for Tanzanian men. They’re not expected to open up and talk about their struggles with life. Every two weeks (Fortnightly), on Wednesdays Michael Baruti and Nadia Ahmed present an episode that will discuss the challenges that men go through and offer detailed insight on mental health for men. If you’re interested in Mental Health and are interested in unpacking and unlearning mental health for men in Tanzania, this podcast is exactly what you need

https://www.menthepodcast.com

subscribe
share






episode 80: Only Way Up


Kutana Babuu wa Kitaa, Super Star, mkali kutoka King’oko, mwana hiphop, na mtangazaji kutoka moja kati ya vyombo vikubwa sana vya habari hapa nchini Tanzania.


Kwa macho ya nje, Babuu ni kijana anayeishi ndoto za watu wengi sana. Kijana, maarufu, ana kazi nzuri, ana familią changa. Nadhani hii ni ndoto ya kila mwanaume. Lakini, kitu ambacho wengi tulikuwa hatukitambui, ni kwamba Babuu anapambana na vita kali sana ndani ya mwili wake na kwenye maisha yake binafsi.


Maisha ya Babuu wa kitaa yalibadilika mara baada ya kugundulika kwamba ana saratanı ya ngozi, lakini pia mmoja kati ya watoto zake watatu anasumbuliwa na “Down syndrome”


Pamoja na yote hayo, Babuu hajakubali changamoto hizi zimrudishe nyuma na kumfanya kuishi kinyonge. Ameendelea kuwa Babuu yule yule ambae wengi tunamfahamu, na kwa sasa anasisitiza kuwa kubali changamoto zako, na njia pekee ya kupambana nazo ni kwa kuangalia na kusonga mbele na juu . “ONLY WAY UP”


Anaketi na Michael pamoja na Nadia, kwa pamoja wanazungumzia vita ya Babuu dhidi ya saratani aliyokutwa nayo, maisha yake kama baba anaelea mtoto ambae yupo tofauti na watoto wengine, na ni vipi ameweza kubaki kuwa Babuu yule yule ambae wote tunamfahamu kati kati ya changamoto zote hizi anazopitia? Na kwanini anaamini sana katika slogan yake ya “ONLY WAY UP”?


Subscribe kwenye channel yetu ya YouTube, utazame na kusikiliza mazungumzo haya ya kusisimua na yenye mafunzo mengi sana kuhusu maisha. 


fyyd: Podcast Search Engine
share








 November 2, 2023  1h20m