Men The Podcast

One of the major barriers to men addressing and tackling the challenges they face is the fact that discussion of mental health is largely taboo for Tanzanian men. They’re not expected to open up and talk about their struggles with life. Every two weeks (Fortnightly), on Wednesdays Michael Baruti and Nadia Ahmed present an episode that will discuss the challenges that men go through and offer detailed insight on mental health for men. If you’re interested in Mental Health and are interested in unpacking and unlearning mental health for men in Tanzania, this podcast is exactly what you need

https://www.menthepodcast.com

subscribe
share






episode 81: Raising a Neurodiverse Child


Mganga hajigangi ni msemo unaofahamika sana na wengi wetu, na wengi tunautumia pale tunapoona inafaa, ila kwa siku ya leo, ni kweli MGANGA HAJIGANGI.


Dr Isaac Maro ni daktari maarufu hapa Tanzania, na amehudumia watu wengi na kutoa ushauri wa kitabibu kwa wagonjwa wengi sana, aidha kwa kupitia taaluma yake kama daktari, kupitia nafasi yake kama mkufunzi wa elimu ya juu, lakini pia kupitia nafasi yake kwenye jamii kama mtayarishaji na muongozaji wa kipindi pendwa cha redio kinachofahamika kama NJIA PANDA.


Lakini, ni nani aliyempa ushauri, na kuwa mganga kwake pale alipogundua kwamba mtoto wake wa pili, Ivan, ana usonji? (Autism). Aliweza kufuata ushauri anaowapa watu wengine au ni kipi alichokifanya ili kuweza kubadili maisha yake na kuendelea kumlea Ivan kwa namna bora?


Kwenye maongezi ya leo, Dr Isaac Maro anachambua changamoto, furaha, mafanikio na yote ambayo mtu anaweza kupitia wakati wa kulea mtoto ambayo ni tofauti na watoto wengine (Neurodiverse) . Lakini pia anajaribu kujibu swali la ipi ni nafasi ya baba kwenye hili, na ni kwanini wanaume wengine hukata tamaa na kuamua kutelekeza familia zao pindi watoto wao wanapokuwa tofauti na watoto wengine.


Karibu kwenye episode ya leo, tujifunze wote. 


fyyd: Podcast Search Engine
share








 November 23, 2023  1h3m