Men The Podcast

One of the major barriers to men addressing and tackling the challenges they face is the fact that discussion of mental health is largely taboo for Tanzanian men. They’re not expected to open up and talk about their struggles with life. Every two weeks (Fortnightly), on Wednesdays Michael Baruti and Nadia Ahmed present an episode that will discuss the challenges that men go through and offer detailed insight on mental health for men. If you’re interested in Mental Health and are interested in unpacking and unlearning mental health for men in Tanzania, this podcast is exactly what you need

https://www.menthepodcast.com

subscribe
share






episode 82: Men and Healing


Katika “episode” yetu ya leo, wanaume wawili wameketi na kuulizana, kweli kuna mwanaume aliyepona? “A healed man”?  Tunaposema “A healed man” au mwanaume aliyepona, hapa tuna maanisha mwanaume ambaye amechukua muda wake kujitambua na kujua mapungufu yake, historia yake, sababu ya kwanini yupo jinsi alivyo, amejifunza kutokana na makosa yake, na pia yupo katika mapambano ya kumfanya awe mwanaume bora zaidi siku za usoni.

 

Kwa mujibu wa mgeni wetu wa leo, ndugu Leslie Omwenga, anasema hakuna kitu kama hicho. Hakuna kitu kama “A healed man”, na sababu kuu ya yeye kusema hivyo ni kwamba anaamini kila mwanaume ana kazi ya kuendelea kupambania afya yake ya akili mpaka siku ya mwisho, hivyo kwake kuna “A healing man”. Au mwanaume anayepona.  Huyu ni mwanaume ambaye kila siku anataka kuendelea kuwa bora, na anatakiwa afanye hivi mpaka siku ya mwisho ya uhai wake.

 

Leslie pamoja na Michael Baruti wanajadili swala hili kiundani, huku kila mmoja akichangia kwenye hili kutokana na uzoefu wake pamoja na ufahamu wake kuhusu mchakato mzima wa kumfanya mwanaume kuwa bora. Hakuna kitu ambacho hakikuguswa hapa, kuanzia malezi, mahusiano, swala zima la kipato, pamoja na swala zima la kumpeleka mwenzi wako ukweni kwake ????????.

 

Karibu katika episode ya leo.


fyyd: Podcast Search Engine
share








 December 7, 2023  1h42m